Monday, February 28, 2011

Kilimanjaro Music Award

KILI AWARDS 2011:Mambo yameiva, kazi kuanza jumatatu!  Send to a friend
Saturday, 26 February 2011 11:27
0diggsdigg
Na Henry Mdimu
Kwa mara ya 12 sasa tunzo za muziki Tanzania, ambazo huwa zinakuja kwa jina la Kilimanjaro Music Awards zinazokuja kwa hisani ya kampuni ya Bia Tanzania, zimewadia, safari hii mawili matatu yakiwa yamebadilika hiuku wasanii mbali mbali wakiwa wameibuka.

Mtoto kama Linah kutoka THT kaonekana sana, 20% naye kaja juu, huku watu wengine kama lady Jaydee wakionekana kama kama kawaida kutajwa tajwa sana kwenye tunzo hizi kutokana na kazi walizoifanyia jamii yao katika medani ya muziki kwa mwaka uliopita wa 2011.

Kuibuka kwa wasanii wapya ni jambo moja lakini jingine ni kuongezeka kwa tunzo ambazo ukiachana na muimbaji Bora, pia mwaka huu msanii bora atatunzwa. waandaaji wamefafanua kwamba kuna tofauti kubwa kati ya muimbaji na msanii linapokuja suala la muziki kwa jamii.
Wataka kujua?

Msanii anafanya mambo mengi, anaimba, anapiga chombo angalau kimoja na hata kama hatapiga chombo lakini angalau anapokuwa jukwaani kuna uchacharikaji unauona moja kwa moja unaendelea pale na kusababisha kuvutia mashabiki wake kuendelea kumuona katika jukwaa, na muimbaji, yeye anaimba tu kwa hiyo si kila muimbaji ni msanii.
Upo?

Hii imekaa kitaalam sana, Reggae na Ragga zimetofautishwa pia ambapo kuna elimu hapa, Reggae ina makundi yake, kuna ile ya kugombania Uhuru kama ya Bob Marley, Lucky Dube na Petter Tosh, lakini pia kuna Sweet reggae, hii kwa ajili ya mapenzi, kama ya akina Gregory Issacs, Maxi Priest, na wengineo, na Ragga ni hii ya majigambo na kufokafoka, ya vijana ni Ragga ya akina Shaba Ranks, Collie Budz, Bennie Man na wengine.

Katika hii hii Ragga pia ina kundi ambalo linatumia maneno makali sana ya ndani ambayo haiwezi kupigwa Redioni, ambayo sasa imepachikwa jina la DanceHall.
Mnaelewa lakini?

Hizi zimewekwa katika makundi mawili.
Reggae imewekwa kwake, ambapo Sweet na ile ya kugombania Uhuru zitakuwa pamoja na na Ragga imewekwa pamoja na Dancehall ili kutoa nafasi zaidi kwa mashabiki wa muziki huu ambao wapo wengi kwa kweli kuweza kupigia kura wasanii wanaowapenda.

mwaka huu hakuna kabisa albam bora, kwa sababu mwaka jana wasanii waliotoa albam sio wengi, hii ni kwa sababu za wasanii wenyewe lakini kwa mujibu wa kamati ni kwamba haya mambo ya albam bora pia yamezua mgogoro, maana kila kundi la muziki sasa lilifikia wakati likawa linadai hii tunzo.

Sasa angalia ukianza kutunza Hip Hop,. Taarab, Zouk, na nyinginezo unahitaji kuwa na Bajeti kubwa sana na kwa kwa Kili Awards ambazo ingawa zinasadikika kuwa ni tunzo za pili kwa ukubwa Afrika, Bajeti bado haijaruhusu kuwa na tunzo zaidi ya hizi 23 zilizopo.

Jambo jingine jipya zuri ambalo tunzo za mwaka huu zitalionja ni ushereheshaji wa wanamuziki wa nyumbani tu, na sio wanamuziki ambao watatoka nje na lengo ni kuwalipa vizuri wanamuziki wa nyumbani ili waijue thamani yao, jambo ambalo wanamuziki wengi wa nyumbani wamelifurahia na wameahidi kufanya maonesho ya kuvbutia kila mtu kwa nafasi yake.
Kura rasmi zitaanza kupigwa jumatatu hii ambapo wasanii watano watano kutoka katika kila aina ya tunzo watawekwa hadharani na mashabiki wataanza sasa kutumia simu, magazeti na vipeperushi kuwapigia kura na mwisho wa safari hii ni tarehe 26 ambapo tunzo zitakabidhiwa.
Starehe Team yatoa kila la kheri katika mchakatio, haki itendeke...

Wednesday, January 13, 2010

Your mostly welcome.....